NIPE MATUMAINI MUZIKI TIBA

Nipe Matumaini, Muziki ni Tiba – “Music is Medicine.”

Karibu kwenye Music Therapy Gala Dinner, tukio maalum linalofanyika katika 4th Public Health Palliative Care Scientific Congress, likiwa na lengo la kuunganisha watu mbalimbali katika kusherehekea nguvu ya muziki katika afya, ustawi na huduma za tiba shufaa.

Nipe matumaini, Muziki Tiba Gala Dinner itawakutanisha watafiti, wataalamu wa afya, watunga sera, waelimishaji, washirika wa maendeleo na jamii kwa ujumla kwa ajili ya jioni ya kujifunza, kushirikiana na kusherehekea nafasi ya muziki katika kuboresha ustawi wa binadamu.

Kupitia kaulimbiu “Muziki ni Tiba”, tukio linaangazia matumizi na umuhimu wa muziki katika pain-free mobility, palliative care, musculoskeletal wellbeing na kuboresha uzoefu wa huduma za afya kwa watu wote.

Taarifa Muhimu

Music Therapy Gala Dinner

  • Tarehe: 1 Oktoba 2026
  • Muda: Saa 11:00 jioni – 4:00 usiku (5:00 PM – 10:00 PM)
  • Mahali: University of Dar es Salaam – New Library
  • Kaulimbiu: Muziki ni Tiba – Music is Medicine

Ni fursa ya kukutana, kujifunza, kushirikiana na kusherehekea nguvu ya muziki katika afya na ustawi wa jamii.

Usikose tukio hili la kipekee. Jisajili sasa na uwe sehemu ya Music Therapy Gala Dinner.

Kwa mawasiliano:   +255 714 510 195 || +255 773 674 376